Ivory coast waichapa Burkina Faso

Haki miliki ya picha AP
Image caption Didier Drogba wa Ivory Coast agonga na Bakary Kone wa Burkina Faso

Ivory Coast jana iliichapa Burkina Faso 2-0 na kufaulu kuingia hatua ya robo fainali ya kombe ya matifa bingwa barani Afrika.

Mshambulizi wa timu ya Chelsea ya Uingereza Salomon Kalou alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 16 pale alipofunga bao.

Na kukuwa kumusalia dakika nane kwa mpira kumalizika Bakary Kone wa Burkina faso alijifunga mwenyewe na kufanya mabao kuwa mbili , bila.

Japo walishinda ,lakini Ivory Coast ambayo ilikuwa na miamba sita wanao sakata boli katika ligi ya Premier ya Uingereza lakini uchezaji wao haukuwa wa kuvutia. Kiuchezaji na kwa umiliki wa mpira , Burkina Faso walikuwa juu.

Kwa kushindwa huko Burkina Faso wamebanduliwa njee ya mashindano hayo.