Blatter awavalia wakuu wa Misri

Rais wa shirikisho linalotawala mpira wa miguu Duniani (FIFA) Sepp Blatter ameshutumu hatua ya Misri ya kuwatimua viongozi wa soka wa nchi hio, akisema kua ni kuingilia kati masuala ya soka na serikali.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sepp Blatter

Blatter anasema ataomba wakuu hao warejeshwe kazini. Aliyasema hayo akiwa katika mji mkuu wa Paraguay ambako anahudhuria kikao maalum cha maofisa wa soka kutoka nchi za Amerika ya kusini. Maofisa hao wanakutana kujadili jinsi ya kuimarisha sheria zinazokinga masuala ya mpira wa miguu yassingiliwe na serikali katika eneo hilo.

Rais wa Chama cha mpira cha Misri na wanachama wake wote walijiuzulu siku ya jumamosi, ingawa walitimuliwa na Waziri mkuu wa Misro kufuatia ghasia zilizozuka kwenye mechi iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 70.

Ghasia hizo zilianza pale mashabiki wa klabu ya Al Masry walipovamia uwanja baada ya timu yao kushinda kwa bao 3-1 dhidi ya Al Ahly kutoka mjini Cairo na kuanza kuwashambulia wapinzani wao.

Mamiya ya mashabiki wa Al-Ahly walisukumwa hadi milango mifinyu ya uwanja ambako walibanwa kwenye milango ya uwanja uliofungwa.

Blatter amesema kua shabaha ya FIFA ni kuulinda mchezo wa soka, kulinda shirikisho na bila shaka kuhakikisha kua hali kama hizo za kuwaingilia maofisa wa mchezo hazirudiwi.

Aliongzea kusema kua watahitaji kikosi cha polisi au jeshi kwa sababu FIFA haina uwezo wa kuingilia kati moja kwa moja.

Mkutano wa shirikisho la Conmebol anaohudhuria Bw. Blatter ulifikia uwamuzi wa kubadili sheria zake ili kupunguza kuingiliwa kwa masuala yake na serikali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nicolas Leoz wa Conmebol

Rais wa Conmebol, Nicolas Leoz kutoka Paraguay alikumbusha tukio la mwaka 2008 nchi ya Peru ilipotimuliwa kutoka uanachama wa FIFA na shughuli zote za soka baada ya serikali kuamuru kua uchaguzi uliomleta madarakani Rais wa Chama cha mpira cha Peru Manuel Burga kwa madai ya rushwa.