Liverpool, Spurs nguvu sawa

Suarez Haki miliki ya picha Getty
Image caption Suarez alirejea baada ya kumaliza adhabu ya kukosa mechi 8

Liverpool imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Spurs wakicheza bila ya wachezaji wao wengi na pia bila ya meneja wao Harry Redknapp, walicheza kufa na kupona kuzuia mashambulizi ya Liverpool yaliyokuwa yakiongozwa na Andy Carroll.

Luis Suarez aliingia muda mchache baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kupata nafasi nzuri, lakini kipa wa Spurs Brad Friedel aliudaka mpira.

Liverpool sasa wanasalia katika nafasi ya saba wakiwa na pointi 39 pointi moja nyuma ya Arsenal. Spurs wamefikisha pointi 50, pointi saba nyuma ya Man City wanaoongoza ligi, na pointi tano nyuma ya Man United waliopo katika nafasi ya poli na pointi 55.

Liverpool watapambana na United Jumamosi.