Huwezi kusikiliza tena

Wanyama akutana na Wanyama

Victor Mugubi Wanyama, ni miongoni mwa wachezaji wachache kutoka Afrika Mashariki wanaosakata kabumbu ya kulipwa katika mataifa ya Ulaya.

Wanyama, mwenye umri wa miaka ishirini na moja, alianzia safari yake huko Ubelgiji, na sasa ni mchezaji wa kiungo cha kati wa kutegemewa na timu ya ligi kuu ya Uskochi ya Celtic.

Katika mazungmzo na mwandishi wa BBC, Wanyama wa Chebusiri, aliyemtembelea mchezaji huyo nyumbani kwake katika mji mkuu wa Uskochi, Glasgow, Wanyama anasimulia juu ya maisha yake.

Zaidi utayasikia katika matangazo yetu ya Michezo na Wachezaji siku ya Jumapili, kuanzia saa tatu usiku za Afrika Mashariki.