Huwezi kusikiliza tena

Victor Wanyama azungumza na BBC

Victor Mugubi Wanyama, ni miongoni mwa wachezaji wachache kutoka Afrika mashariki wanaosakata kabumbu ya kulipwa katika mataifa ya Ulaya.

Wanyama, mwenye umri wa miaka 21, na alianzia safari yake huko Ubelgiji na sasa ni mchezaji wa kiungo cha kati wa kutegemewa na timu ya ligi kuu ya Uskochi ya Celtic.

Ameichezea Celtic sasa kwa muda wa miezi sita.

Katika mazungmzo na mwandishi wa BBC, Wanyama wa Chebusiri aliyemtembelea mchezaji huyo nyumbani kwake katika mji wa Glasgow, Victor Wanyama anaeleza hana nia ya kuhamia England kwa hivi sasa.