Blackstars wagawanyika kwa uchawi

Kocha wa Timu ya Taifa ya Ghana Goran Stevanovic amesema kua mgawanyiko uliojitokeza katika kikosi cha Timu hio umetokana na baadhi ya wachezaji kuwatendea wenzao uchawi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha Stevanovic wa Ghana

Mserbia huyo alitoa madai hayo katika taarifa iliyovuja kuhusiana na sababu zilizoikosesha ufanisi Timu ya Black Stars kwenye mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012, walipolazwa na Zambia katika nusu fainali.

Katika taarifa iliyowasilishwa kwa wakuu wa chama cha mpira cha Ghana, Stanovic aliongezea kusema kua ''baada ya kupoteza pambano dhidi ya Zambia, wachezaji walirushiana lawama miongoni mwao.

Hata hivyo Kocha huyo hakutaja majina ya wahusika katika taarifa yake na Chama cha mpira kimekataa kutoa taarifa yoyote, kwa kusema hakijadili masuala yanayotoka kwenye taarifa zilizovuja.

Sarfo Gyami, aliyeshiriki Kombe la Mataifa la mwaka 1992 ameiambia BBC michezo kwamba, hakuna geni hapa ila wachezaji hutumia dawa hii kama kinga kwao binafsi.

Mchezaji huyo wa zamani aliongezea kusema kua hajawahi kusikia kua kuna wachezaji wanaotumia uchawi kuwaroga wenzao.

Timu ya Black Stars ilitoa sura ya umoja kwenye kombe la Mataifa ya Afrika ambapo video na picha za hali hio pamoja na wachezaji wakiimba kusambazwa kutoka kambi ya timu hio.

Lakini sasa kocha Stevanovic na Rais wa GFA chama cha soka Ghana Kwesi Nyantakyi wanakiri kua kweli kuna mgawanyiko.