Kenya yashinda,Uganda yafungwa

Katika michezo, matokeo ya mechi zilizochezwa leo katika kinyanganyiro cha kuchuja Timu zitakazoshiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huko Afrika kusini mwaka 2013, Madagascar imechapwa na Cape Verde 4-0.

Tanzania ikasabishwa sare ya 1-1 na Msumbiji mjini Daresalam.Rwanda ikaharibu mipango ya Nigeria kwa kutoa sare ya kutofungana 0-0, Ethiopia ikatoa sare ya 0-0 na Benin mjini Adis Ababa.

Burundi ikaichapa Zimbabwe 2-1 mjini Bujumbura. Mjini Nairobi, Kenya ikafanikiwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Togo. Mjini Ndjamena Chad ikaitoa Malawi 3-2. Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ikaanza vizuri kampeini kwa kuinyunyizia Ushelisheli 4-0. Juhudi za Uganda katika kipindi cha kwanza kuishinikiza Congo Brazzaville mjini Brazaville ziliichosha na kuchapwa 3-1.

Katika michuano kama hio kwa bara Asia, Saudi Arabia imeondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 2014 kwa kipigo cha mabao 4-2 na Australia huku Oman ikisonga mbele kuingia hatua za mwisho za Timu kutoka bara Asia.

Timu nyingine ngumu kutoka eneo hilo Korea ya kusini imepona aibu kama Saudi Arabia kwa kuichapa Kuwait 2-1 na Qatar ikapata bao la dakika za majeruhi kusawazisha mawili ya Iran licha ya Bahrain kuinyunyizia Indonesia mabao 10-0.

Bahrain ilihitaji mabao 8 na Qatar ipoteze mechi yake ili iweze kusonga mbele lakini Qatar ilijizatiti na kupata mabao mawili dhidi ya IRAN ambayo tayari ilikua imeisha fuzu