Man.united ina kibarua

Meneja wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amebashiri kua mchuano wa klabu yake dhidi ya Tottenham siku ya jumapili ndiyo mchuano mgumu katika jitihada za kutetea taji la klabu yake na kuingoa Man.city kutoka kileleni.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Sir Alex Ferguson

Licha ya wasiwasi huo United haijapoteza mechi katika mechi 25 ilizopambana na Tottenham tangu mwezi May 2001. Pamoja na historia kuipendelea United mshambuliaji wake Wayne Rooney atarejea kwa pambano hilo baada ya kukosa mechi mbili akiumwa koo.

Tottenham ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester United ndiyo bado imechapwa na Arsenal 5-2 ikimkosa kiungo wake Scott Parker anayetumikia kifungo cha kadi nyekundu.

Kutokuepo kwa kiungo Parker ni pigo kubwa kwa Spurs, amesema meneja wa klabu hio Harry Redknap.

Hata hivyo mtaalamu huyo wa soka anasema ataziba mapengo hayo kwa kutumia wachezaji kama Sandro na Jake Livermore ikiwa fursa kwao kuonyesha uwezo wao.

Tabia ya kuziba mapengo si tatizo kwa United ambayo inakumbuka Willem Korsten aliyefunga mawili kwenye uwanja wa White Hart Lane kuipa Spurs 3-1 dhidi ya Timu ambayo tayari ilikua imeisha tangazwa mshindi wa Ligi ya mwaka 2000-01

Ryan Giggs na Paul Scholes wote walishiriki pambano hilo na huenda wakawepo jumapili wakati Giggs akisherehekea mechi yake ya 900 akichezea.