Scolari asema Chelsea ni "jehanam"

Kufanya kazi chini ya Roman Abramovich itakuwa sawa na kuingia "jehanam" kwa meneja mpya wa Chelsea, kwa mujibu wa meneja wa zamani wa klabu hiyo Luiz Felipe Scolari.

Image caption Luiz Filipe Scolari amuonya atakaye vaa viatu vya Villas-Boas

Abramovich kwa sasa anamtafuta meneja wa nane wa kudumu tangu mwaka 2003 baada ya kumtimua Andre Villas-Boas siku ya Jumapili.

"Itakuwa sawa na kuingia kuzimu kwa yeyote atakayechukua nafasi ya Villas-Boast," alisema Scolari,ambaye aliwahi kuwa meneja wa Chelsea kwa miezi saba kati ya mwaka 2008-09.

"Kumtimua lilikuwa jambo la ajabu, ingawa si ajabu sana kwangu kwa sababu ya kile nilichokumbana nacho nilipokuwa katika klabu ile.