Barcelona wako sayari tofauti

Messi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lionel Messi

Nahodha wa klabu ya Ujerumani, Bayer Leverkusen Simon Rolfes amesema kua klabu ya Barcelona imo katika sayari tofauti na wengine ambapo klabu hio ya Uhispania inatetea taji ililoshinda mwaka uliopita.

Mabingwa hao waliisasambua Leverkusen kwa kuikandika 7-1 huko Barcelona jumatano usiku kuingia robo fainali za mashindano ya vilabu.

Baada ya kuichapa Manchester United 3-1 kwenye uwanja wa Wembley na kushinda Kombe la Msimu uliopita Barcelona inajitahidi kua klabu ya kwanza kushinda Kombe hilo kwa misimu inayofuatana.

Nyota wa klabu hio na mchezaji bora wa mwaka Duniani, akiwa bado na umri mdogo wa miaka 24, Lionel Messi, aliweka rekodi mpya kwa kufunga mabao matano dhidi ya Wajerumani walioonekana kuishiwa maarifa wakiondolewa kwenye hatua hii kabla ya robo kwa jumla ya mabao 10-2.

Messi alifunga mawili kabla ya mapumziko na baadaye kuongezea matatu huku kijana chipukizi Cristian Tello akifunga mawili kabla ya Karim Bellarabi kufunga la Leverkussen la kufutia machozi.

Mcheza kiungo wa Timu ya Taifa ya Ujerumani Rolfes aliutaja mchuano huo kama kizaizai''

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lionel Messi

Mchezaji huyo aliwataja Messi, Xavi na Andres Iniesta kama balaa wanaposhambulia.

Si rahisi kuondoka ndotoni baada ya kipigo kama hicho, hatukutaka matokeo kama hayo, lakini tulizidiwa, alimalizia mchezaji Rolfes.'