Msimu wa Magari ya Langalanga

McLaren
Image caption Hamilton wa McLaren

Kuna nadharia kwamba mashindano ya mbio za magar za Langalanga yanapaswa kua kilele cha ujasiri, muundo wa gari zuri la kuvutia na urembo wake kuambatanisha ushindi.

Lakini dhana hio imenadilika kwa sababu takribana magari yote yanayotazamiwa hayana sura ya kuvutia.

Timu mbili ambazo kwa njia nyingine zimekua na mafanikio kwa kua ndiyo bado magari yao yana sura ya kuvutia kama McLaren na Red Bull.

Kishindo cha ushindani

Sebastian Vettel wa Timu ya magari ya Red Bull, akiwa ndiye bingwa mtetezi kwa miaka miwili mfululizo mwenye umri mdogo kuwahi kufanya hivyo katika historia ya mbio hizi, hajapoteza ujasiri wake.

Chipukizi katika mashindano haya ni Mbrazil,Bruno Senna - mwipwa wa marehemu Ayrton Senna -ambaye wakati wake alitia for a kabla ya ajali wakati wa mashindano, ametia saini kuiwakilisha Timu ya magari ya Williams kwa mwaka 2012.

McLaren

Hata hivyo Timu ya McLaren inaonekana kua imeunda gari jipya ambalo madereva wake Jenson Button na Hamilton wanaweza kumshinda Mjerumani.

Hamilton anasema kua mazowezi aliyoyafanya kupitia kipindi cha majira baridi katika milima ya Rocky huko Colorado yamemuondolea mashetani yaliyomsababisha kupata ajali mara kadhaa kuliko ushindi aliopania mwaka jana.

Maridhiano na mpenzi wake muimbaji Nicole Scherzinger nalo ni suala linaloweza kumsaidia kutulia kiakili.

Ushindani wa ndani baina ya Button na Hamilton unaweza kua sehemu ya pambano kubwa la mbio hizi na kufuatiliwa kwa makini.

Hapana shaka yoyote kua Hamilton ndiye dereva mwenye kasi kumzidi mwenziye Button, ingawa kua hisia kwamba Button ndiye mtulivu zaidi anayekubaliana na sheria mpya za F1 -hususan kuhusiana na tairi za Pirelli zeye sifa ya kuishilia haraka.

Kwenye mbio za msimu huu Hamilton anataka kuthibitisha kua hayo yote hayana ukweli na bila shaka ataonyesha kwa matokeo ya uhakika kwa kipindi kisicho kifupi cha mashindano.

FERRARI Kama wewe umekua ukifuatilia mashindano ya mpira wa aina moja au nyingine kipindi cha majira ya baridi basi utakua ulikosa kufuatilia juhudi na utabiri wa Timu ya magari ya Ferrari kua zamu hii watamkabidhi dereva wao Fernando Alonso gari ambalo halihitaji bahati ili kushinda mbio kuanzia mwanzo hadi mwisho wa msimu.

Rais wa Timu ya Ferrari Luca di Montezemolo ameonyesha kua na matumaini kua mambo hayatokua mabaya kama wengi wanavyodhani. Lakini amebainisha kua anataka matokeo mazuri na majibu, kwa haraka.