Inter yahitaji damu mpya

Kundi la wachezaji ambao mda wao unayoyoma kwa klabu ya Inter Milan na mageuzi yanatarajiwa baada ya mabingwa wa mwaka 2010 wa Ligi ya mabingwa kutupwa nje na Olympique Marseille.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Wesley Sneider

Rais wa klabu hio Massimo Moratti alimuondolea makosa kocha Claudio Ranieri kufuatia mchuano wa jumanne kutokana na magoli ya ugenini.

Mchuano huo ulimalizika 2-2 baada ya Inter kushinda nyumbani 2-1, lakini bao la ugenini likabadili matokeo na hivyo kuashiria kua Inter msimu huu inaondoka kapa bila Kombe hata moja.Klabu hio imeisha ondolewa katika mashindano ya Kombe la Italia ikiwa ya saba kwenye msimamo wa Ligi ya Serie A.

Hali hii ilianza punde baada ya kocha wao Jose Mourinho kuondoka kufuatia ushindi wa makombe matatu miaka miwili iliyopita.

Mreno huyo mjanja alifahamu vyema umri wa kikosi cha Inter kua hautoiwezesha kufikia kiwango hicho tena na kuondoka na heshima yake.

Rafa Benitez akafuata kujaribu bahati yake, akashindwa na Leonardo akamrithi naye akianguka, kisha akaja Gian Piero Gasperini na baada ya kushindwa ndio akateuliwa Ranieri.

Rais wa Inter amesema haifai kufikiria mageuzi bali ni marekebisho.Sidhani kama kocha ana tatizo, angalau hadi mwisho wa msimu.