Button ashinda Australia

Button Haki miliki ya picha Getty
Image caption Button aanza vyema msimu

Jenson Button wa Timu ya magari ya McLaren ameshinda mbio za kwanza msimu huu huko Australia akimpiku Lewis Hamilton aliyetangulia kwenye jukwaa na kumaliza mbio katika nafasi ya tatu.

Button, aliyefuzu kwa mbio za leo katika nafasi ya pili nyuma ya Hamilton alimpita kwenye kona ya kwanza na kushikilia uongozi hadi mwisho.

Hamilton aliipoteza pia nafasi ya pili kwa Sebastian Vettel wa magari ya Red Bull kufuatia mbio hizo kukatizwa na gari la usalama wakati Mjerumani akiingia baada ya kusimama katika kituo cha mafuta.

Mark Webber wa Timu ya Red Bull alimaliza wa nne mbele ya Fernando Alonzo ambaye aliendesha kwa kasi mashindano haya.

Button aliendesha gari lake bila kufahamu sakata inayoendelea nyuma yake akiwa peke yake baada ya kuanza vyema na kumpita Hamilton kwenye kona ya kwanza.

Baada ya mbio hizi Button alisema kua "inaonyesha kua mapumziko ya majira ya baridi ni muhimu yametuwezesha kujikusanya na haya ndio matunda yake.

Hamilton hakuwa na mengi ila kusema tu kua haikua siku yangu. La muhimu ni kuendelea na juhudi na siku yangu itafika.