QPR yazima jazba la Liverpool

Meneja wa klabu ya QPR Mark Hughes ameshukuru ushindi wa kimiujiza dhidi ya mojapo ya vilabu vikuu katika Ligi ya England, Liverpool.

Haki miliki ya picha
Image caption Mark Hughes wa QPR

Katika mchuano uliofanyika kwenye uwanja wa QPR mjini London Liverpool ndiyo iliyopata bao kwanza kupitia Sebastien Coates baada ya kumiliki mchezo kwa kipindi kirefu.

Dirk Kuyt aliongeza bao la pili ikiwa zimesalia dakika 20 ambapo baadhi ya mashabiki wa QPR walianza kuondoka uwanjani kuepuka mabao zaidi ya Liverpool.

Lakini wachezaji wa QPR walikua na mtazamo tofauti kuhusu matokeo kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Mshambuliaji wa QPR Shaun Derry alitikisa nyavu za Liverpool na kuamsha matumaini ya angalau pointi moja kwa klabu yake iliyokua njia panda ya kushuka daraja.

Bao hili liliwachangamsha washambuliaji na timu nzima ambapo mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Djibril Cisse aliruka na kuuchupa mpira huhesabu la pili la QPR kabla ya Jamie Mackie kuuzima uwanja kwa mkwaju wa chini kumpa matumaini Meneja Mark Hughes ya kusalia katika Ligi ya Premiership mwakani.

Meneja Hughes mwenyewe alisema baada ya mechi hio kua huo ni mwanzo wa utekelezaji wa kazi kubwa iliyo mbele yao.