Mancini asema ushindi mnono

Mancini na Tevez Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mancini na Tevez

Carlos Tevez alirejea kutoka uhamishoni kumtengenezea fursa Samir Nasri kufunga bao la dakika ya mwisho katika ushindi dhidi ya Chelsea.

Vijana wa Roberto Mancini walikua tayari wanaliona Kombe la Ligi likiwaaga baada ya Gary Cahill kupiga shuti lililowagonga ndugu wawili Yaya na Kolo Toure kugongwa na mpira uliomchanganya goalkeeper na kuhesabu la kwanza kwa Chelsea ikiwa dakika ya 60.

Hio ikawa ishara kwa Mancini kumleta aliyekua msaliti Tevez kwa mara ya kwanza tangu mwezi Septemba ilipodaiwa kua alikataa kuingia uwanjani kusaidia kubadili matokeo ya mechi dhidi ya Bayern Munich nchini Ujerumani.

Aliingia na kuwakumbusha mashabiki nini walikikosa kwa kipindi kirefu na yeye mwenyewe alichokikoa kwa mda wote huo.

Ushindi wa City uliiweka klabu hio pointi moja nyuma ya mahasimu wao Manchester United ambayo itatembelea uwanja wa Etihad mnamo mwezi April.

Alikua Sergio Aguero aliyefunga bao la City kwa mkwaju wa peneti baada ya Michael Essien kuunawa mpira katika eneo la hatari. Huu ukawa ushindi wa mara ya 20 wa City kwenye uwanja wao wa Ettihad msimu huu.

Kaskazini mwa London Meneja wa Tottenham hotspurs Harry Redknapp anasema kua klabu yake imepoteza muelekeo baada ya mechi nne bila ushindi.

Sare ya 1-1 dhidi ya Stoke siku ya jumatano umebadili msimamo kwa kuiweka klabu hio nyuma ya mahasimu wao wakuu Arsenal.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Harry Redknapp

Redknapp anasema ni vigumu kueleza tatizo lilipo kwa wakati huu lakini lazima tuamke kujiandalia mchuano dhidi ya Chelsea jumamosi.

Hadi Februari mosi Tottenham iliongoza hasimu wake Arsenal kwa tofauti ya pointi 12 na ubishi ulizuka kama Tottenham sasa imepata dawa ya kua Timu bora ya jiji la London na bora kuliko Arsenal.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Arsene Wenger

Kwa upande wake Arsenal iliendelea kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Everton.

Licha ya ushindi huo Meneja Arsene Wenger amewaonya wachezaji wake wasidorore hata mara moja katika michuano iliyobaki ili kusalia katika nne bora na kuhifadhi nafasi ya tatu ili iweze kushiriki michuano ya Ligi ya mabingwa mwakani.

Wenger alisema baada ya mchuano huko Goodison park "tumejiwekea hali nzuri na mazingira ambayo tunataka tuhifadhi hadi mwisho.

Arsenal imepitia kipindi kigumu msimu huu ikiwa ni pamoja na mwezi januari ilipopoteza mechi tatu za Ligi kuu dhidi ya Fulham,Swansea na Manchester United.