Beki Pepe aona nyekundu

Pepe Haki miliki ya picha AP
Image caption Pepe

.Beki wa klabu ya Real Madrid Pepe amepewa adhabu ya kutoshiriki mechi mbili za Ligi ya La Liga kwa kumtukana mwamuzi kufuatia sare ya 1-1 siku ya Ijumaa klabu hio ikichuana na Villarreal.

Mwenzake Sergio Ramos, hata hivyo aliponyoka adhabu kubwa baada ya adhabu ya kadi ya njano aliyoonyeshwa siku ya jumatano kupuuzwa na Kamati ya shirika la mpira la Uhispania.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mourinho si mgeni kwa kadi nyekundu

Beki huyu wa Real Madrid ataweza kushiriki mechi dhidi ya Real Sociedad siku ya jumamosi.

Kocha Jose Mourinho na mcheza kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil walionyeshwa kadi nyekundu wakati wa pambano hilo, baada ya Villarreal kunyakua bao lake la kusawazisha, pia walipewa adhabu ya kikwazo cha mechi moja.

Msaidizi wa Mourinho Rui Faria alipewa adhabu ya kikwazo cha mechi mbili baada ya kuamrishwa aondoke katika handaki la uwanjani katika kipindi cha pili huko Madrigal.