United yaizaba Blackburn

Valencia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Valencia alipachika bao la kwanza

Manchester United imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi kuu ya England baada ya kuizaba Blackburn Rovers kwa mabao 2-0.

Man United wakicheza ugenini walibanwa kwa takriban dakika 80.

Antonio Valencia ndiye aliandika bao la kwanza la United baada ya kuachia mkwaju mkali kutoka upande wa kulia.

Dakika tano baadaye, Ashley Young aliyeingia badala ya Paul Scholes alifunga bao maridadi na kuhakikishia United pointi tatu muhimu katika mbio za kutetea ubingwa wao.

Blackburn imerejea katika nafasi ya kumi na nane.