Kenny Dalglish hataondoka Liverpool

Kenny Dalglish hatang'atuka katika nafasi yake ya umeneja wa Liverpool, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani katika klabu hiyo Mark Lawrenson.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kenny Dalglish huenda asitimuliwe LIverpool

Liverpool ilishinda Kombe la Carling na kwa sasa imo katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA, lakini kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Newcastle kilikuwa cha sita kati ya michezo saba ya Ligi Kuu ya Kandanda ya England.

Lawrenson, ameiambia BBC:"Sidhani kama ataondoka."

"Siamini pia kama atatimuliwa. Matokeo ni mabaya, lakini wamiliki hawatachukua uamuzi mkali dhidi yake."

Liverpool, ambao wameporomoka hadi nafasi ya nane ya msimamo wa ligi, itakumbana na mahasimu wao wakubwa kutoka mji mmoja Everton katika kipute cha nusu fainali ya Kombe la FA tarehe 14 Aprili.

Lawrenson ameongeza: "Wanaweza kushinda Kombe la FA msimu huu, ambapo watakuwa wameweka kibindoni makombe mawili na litakuwa jambo la ajabu kumtimua meneja.

"Ukiwa meneja katika Ligi Kuu, ni balaa kubwa timu yako inapopoteza michezo kadha.

"Wataikaribisha Aston Villa mwishoni mwa wiki na nisingependa kusema ni mechi ya kufa na kupona kushinda, lakini ndivyo ilivyo. Natumai Dalglish atakuwa sawasawa, lakini kwa kiwango chochote lazima ushinde mechi."

Lawrenson amebainsiha tatizo ni kukosekana kwa kile kilichotarajiwa kutoka kwa akina Andy Carroll, Charlie Adam, Stewart Downing na Jordan Henderson, wachezaji walionunuliwa kwa kitita kikubwa na Dalglish cha jumla ya paundi milioni 85.

"Tatizo kubwa ni Adam, Downing, Carroll na Henderson ambapo miongoni mwao wameweza kuchangia mabao sita ya michezo ya ligi," alisema Lawrenson. "Hapo unatazamia mabao kati ya 25-30 miongoni mwao.