Esperance kupambana na Brikama

Harrison Afful Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabingwa watetezi Esperance wanatazamia mno kuingia raundi ya pili ya mechi za klabu bingwa Afrika

Mabingwa watetezi wa ligi ya klabu bingwa barani Afrika, Esperance ya Tunisia, wanatumaini kufuzu kuingia raundi ya pili ya mashindano hayo, baada ya mechi ya Ijumaa dhidi ya Brikama United ya Gambia.

Iwapo mechi itakwisha kwa kutofungana, bado timu hiyo ya Tunisia itafuzu, kwa kuwa awali walifanikiwa kuishinda Brikama United walipocheza Gambia.

Walipokutana mara ya kwanza, mechi ilikwisha kwa sare ya 1-1.

Watakuwa chini ya kocha Faouzi Benzarti, ambaye kwa mara ya nne, alikabidhiwa kibarua cha kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita.

Timu nyingine ya Tunisia, Etoile du Sahel pia wako uwanjani Ijumaa dhidi ya APR.

Ikiwa mechi hiyo itakwisha kwa sare ya magoli, basi wageni Rwanda watafuzu kuendelea katika mashindano hayo, kwani timu hizo zilipokutana katika mkondo wa kwanza mjini Kigali, Rwanda, mechi ilikisha 0-0.

Mechi ya tatu ya Ijumaa ni ya nchini Sudan, wakati Al Hilal itaikaribisha uwanjani DFC 9eme Arrondissement, ambayo pia hujulikana kama Diplomats, kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wageni Diplomats tayari ni dhaifu, kwani walifungwa magoli 3-0 walipocheza na Al Hilal katika mechi ya kwanza.