Arsenal Chelsea nguvu sawa

Arsenal Haki miliki ya picha Getty
Image caption Timu zote mbili zilipoteza nafasi kadhaa

Arsenal imegawana pointi na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates baada ya kutoka sare ya 0-0.

Chelsea wakiwa na mechi ngumu dhidi ya Barcelona siku ya Jumanne, walichezesha wachezaji kadhaa wa akiba ili kujaribu kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya.

Licha ya nafasi za hapa na pale kutoka pande zote mbili, mchezo huo ulikosa msisimko mkubwa kutokana na wachezaji kupoteza pasi na mipira kila mara.

Matokeo haya yanaiacha Arsenal katika nafasi ya tatu, ingawa matokeo ya Tottenham na Newcastle huenda yakaipa wasiwasi klabu hiyo ya kaskazini mwa London.