Vettel ashinda Bahrain

Sebastian Vettel Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bingwa wa dunia Sebastian Vettel alipata ushindi katika mashindano ya Bahrain

Bingwa wa dunia Sebastian Vettel kutoka Ujerumani, na wa timu ya Red Bull, ameibuka bingwa katika mashindano ya Jumapili ya magari ya Formula One mjini Manama, Bahrain.

Vettel amepata ushindi huo huku malalamiko makali ya kisiasa dhidi ya uongozi wa nchi hiyo ukiendelea, na waandamanaji wakisema kabisa haikufaa familia katika uongozi wa nchi hiyo, na iliyozima maandamano ya kisiasa mwaka uliopita, kuruhusiwa kuandaa mashindano hayo.

Ulinzi mkali uliwazuia waandamanaji kufika karibu na barabara zilizotumiwa katika mashindano hayo.

Kimi Raikkonen, wa timu ya Lotus, na kutoka Finland, alimaliza katika nafasi ya pili.

Mwenzake katika timu ya Lotus, Romain Grosjean alishikilia nafasi ya tatu.