Van Persie mkutanoni

Mshambuliza wa Arsenal Robin van Persie aanza gumzo la na wakuu wa klabu hiyo kuhusu hatma yake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Van Persie kukutana na Wenger kuhusu Mkataba wake

Mwamba huyo anatarajiwa kukutana na Meneja Arsene Wenger na halikadhalika Mkurugenzi wa Arsenal Ivan Gazidis siku ya Jumatano.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika nyumbani kwa Wenger.

Lakini haionekani kama muafaka wowote utafikiwa kabla ya siku ya Alhamisi ambapo Van Persie anatarajiwa kujiunga na timu yao ya taifa ya Uholanzi.

Mchazaji huo mwenye umri wa miaka 28 amesalia na mwaka mmoja kabla ya kandarasi yake na Arsenal kumalizika.

Van Persie ndie nahodha wa klabu ya Arsenal na pia alichaguliwa mfungaji bora wa msimu huu katika ligi kuu ya uingereza.