Aston Villa yampata Paul Lambert

Paul Lambert Haki miliki ya picha AP
Image caption Paul Lambert

Klabu ya Aston Villa imethibitisha kua aliyekua meneja wa Klabu ya Norwich City Paul Lambert ameteuliwa kua meneja wake mpya.

Lambert mwenye umri wa miaka 42, anachukua nafasi iliyokua ya Alex McLeish, aliyetimuliwa siku moja baada ya mechi ya mwisho wa msimu.

Lambert aliiongoza Norwich kupanda kutoka daraja la Ligi ya kwanza na katika msimu wake wa kwanza katika daraja la Ligi kuu klabu hio ilimaliza ya 12 .

Huyu atakua meneja wa nne wa klabu ya Villa katika kipindi cha miaka miwili.

Taarifa ya klabu ya Aston Villa imethibitisha na kusema kua ''Bodi ya Aston Villa ina furaha kutangaza na kuthibitisha kua Paul Lambert ameteuliwa kama meneja."

Lambert, aliyeomba kujiuzulu kutoka Norwich siku ya Ijumaa alishangazwa kuona akikataliwa na Norwich".Paul Lambert