Redknapp njia panda kuhusu Spurs

Harry Redknapp Haki miliki ya picha
Image caption Harry Redknapp

Nafasi ya Meneja wa Tottenham kama kiongozi wake inazidi kua tete licha ya mkongwe huyo kukana kua atajiuzulu.

Redknapp, mwenye umri wa miaka 65, alitazamiwa kukutana na Mwenyekiti wa Klabu hio Daniel Levy, kujadili majaliwa yake.

Inafahamika kua Wakuu hao hawajawezxa kuafikiana juu ya mapatano ya mkataba mpya, ambapo Mkataba wa Redknapp unamalizika Juni 2013.

Mwenyekiti wa Klabu Levy inaaminika kua hakuelewa sababu za timu yake kudorora mwishoni mwa msimu.

Haya yanatokea baada ya Redknapp kukanusha kua alijiuzulu n kukiambia kituo cha runinga cha ESPN kuwa hajajiuzulu.

Meneja huyo aliyeiwezesha klabu hio iweze kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza mwaka 2010, alisema kua jambo la kuridhisha ni kwamba bado nina mwaka mzima kwwenye mkataba huo.

Huku nyuma mahasimu wa Klabu ya Spurs, Arsenal inaeleweka wana karibia kumsajili mshambuliaji kutoka klabu ya Montpellier akichezea Timu ya Ufaransa Olivier Giroud KWA makubaliano ya kitita cha pauni milioni £12.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Olivier Giroud

Arsenal inatarajiwa kumtangaza kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 baadaye wiki hii.

Imearifiwa kuwa Meneja Arsene Wenger ana nia ya kumchezesha kijana huyo karibu na Podolski na mshambuliaji Robin van Persie kwenye safu ya washambuliaji watatu.

Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 3 hakushiriki mchuano wa Ufaransa dhidi ya England, lakini ana sifa ya kufunga jumla ya goli 21 zilizoisaidia klabu yake kushinda Ligue ya kwanza nchini Ufaransa.

Giroud ni mmoja wa washambuliaji maarufu katika kikosi cha Ufaransa pamoja na Karim Benzema. Ameiwakilisa nchi yake mara sita na kufunga bao moja,

Mapema wiki hii Meneja wa klabu ya Montpellier Rene Girard alikiambia kituo cha Rediyo huko Ufaransa RMC kuwa Wenger anaongoza msafara wa wakuu wa vilabu vikuu vinavyomtaka mchezaji huyo.

Girard alisema; "Arsenal wanamtaka na yeye Giroud anataka kushiriki Ligi ya England, endapo Arsene atakubaliana na Rais wa Montpellier basi atatia saini mkataba na kua mchezaji wao.

Ingawa zimekuwepo tetesi kuhusu majaliwa ya Van Persie, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao, inafahamika kua Arsenal inamsajili Giroud kucheza pamoja naye na sio mrithi wake.