Sweden yaondoka kwa kishindo

Ufaransa na Sweden Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wafaransa itawabidi kucheza kwa hima zaidi watakapokutana na Uhispania

Bao lililoingia wavuni kwa ustadi kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic limeisaidia Sweden kuishinda Ufaransa magoli 2-0 katika mechi ya kundi D usiku wa Jumanne, na kuhakikisha wameisukuma Ufaransa katika nafasi ya pili katika kundi, na pia kuilazimisha kukutana na mabingwa watetezi Uhispania katika mechi ya robo fainali ya Euro 2012.

Ufaransa walilemewa katika mechi hiyo, na Ola Toivonen alikaribia kuiletea Sweden bao la kwanza alipogonga sehemu ya nje ya mwamba wa goli.

Hatimaye Ibrahimovic alipata bao kupitia mkwaju kutoka yadi 15, baada ya kusukumiwa mpira kutoka kwa Sebastian Larsson.

Olivier Giroud alifunga kwa kichwa na kuiwezesha Sweden kupata bao lao la pili.

Kushindwa kwa Ufaransa kuna maanisha hatua yao ya kucheza pasipo kushindwa katika msururu wa mechi 23 zilizopita tangu waliposhindwa wakiwa nyumbani na Belarus mwezi Septemba mwaka 2010 imesitishwa.

Huo ndio muda mrefu zaidi ulioandikishwa timu kucheza pasipo kushindwa kwa upande wa mechi za kimataifa.

Ufaransa wameshindwa baada ya mechi 24 za kimataifa, na kocha Laurent Blant sio tu atakuwa na wasiwasi katika kupambana na mabingwa wa Ulaya na wa dunia pia, bali pia kuhusiana na timu yake kucheza mchezo wa kiwango duni.

Sweden tayari walikuwa wameondolewa katika mashindano baada ya kushindwa katika mechi zao mbili za mwanzo, lakini nia yao ilikuwa ni kucheza kadri ya uwezo wao kabla ya kurudi nyumbani.

Jumapili iliyopita, wachezaji hao walikataa ushauri wa meneja Erik Hamren wa kupumzika, na badala yake waliamua kuitumia siku hiyo katika kufanya mazoezi zaidi.