Dame Ndoye hatashiriki Olimpiki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Dame Ndoye

Kilabu moja ya soka nchini Denmark, "Copenhagen" imekataa kumruhusu mchezaji wa kilabu hiyo Dame Ndoye kuweza kushiriki michezo ya Olimpiki.

Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Senegal, alitajwa kama mmoja wa wachezaji watatu walio na umri mkubwa kuweza kuchezea timu ya Senegal ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 23 kwenye Olimpiki.

Kulingana na sheria za shirikisho la soka duniani, Fifa, vilabu ndio vina jukumu la kuwapa ruhusa wachezaji walio na umri mkubwa kushiriki kwenye Olimpiki.

Rais wa shirikisho la soka nchini Senegal, Augustin Senghor aliambia BBC kuwa mchezaji mwingine Kalidou Yero Coulibaly mwenye umri wa miaka 21 kutoka kilabu ya Gil Vicente nchini Ureno atachukua nafasi ya Ndoye.

Mechi za Senegal

Tarehe 26 Julai itacheza dhidi ya UingerezaTarehe 29 Julai itamenyana na Uruguay.Tarehe1 mwezi Agosti, itatoana kijasho na United Aarab Emirates.

Yero alikuwa mmoja wa wachezaji wa akiba waliokuwa wametajwa katika kikosi cha Senegal kitakachoshiriki michezo ya Olimpiki.

Senegal wataendelea na maandalizi yao ya michezo ya Olimpiki Jumanne wiki ijayo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uswizi, ambao pia walifuzu kushiriki michezo hiyo.

Kikosi cha Senegal kitakuwa kifua mbele wakati kikijiandaa kwa mechi hiyo ya kirafiki na Uswizi hasa baada ya kushinda Uhispania mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki siku ya Ijumaa.

Hii ina maana kuwa Senegal wana wachezaji wawili tu walio na umriu mkubwa wala sio watatu kama inavyoruhusiwa, Mohamed Diame, 25 anayechezea West Ham United na Papa Gueye, 28, wa kilabu ya Metallist Kharkiv nchini Ukraine.