Mwanariadha huru kushiriki London 2012

London 2012 Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mwanariadha kushiriki chini ya bendera ya IOC

Bodi ya kamati kuu ya shirika hilo imekubaliana leo kumruhusu Guor Marial ashiriki mashindano ya mwaka huu kama mwanariadha huru.

IOC linasema kuwa Marial hana pasi na hawakilishwi na chama chochote cha Kitaifa cha Olimpiki. Nchi alikozaliwa ilijipatia Uhuru wake mwaka jana baada ya kujikwamua kutoka Sudan.

Sudan ya kusini hadi sasa haijakubalika na haina kamati ya Olimpiki inayotambulika.

Haki miliki ya picha AP
Image caption London 2012

Marial alihamia Marekani kama mkimbizi akiwa bado mdogo.

Guor alifuzu kwa kufikia kiwango kinachohitajika kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa kumaliza mbio za marathon katika mda wa saa 2, dakika14, na sekunde 32 mwaka 2011. Tangu hapo ameweka mda bora.

Msemaji wa IOC Mark Adams anasema tukio hili ni la kwanza kujitokeza katika historia ya michezo ya Olimpiki.Shirikisho la kimataifa linalosimamia michezo ya Olimpiki (IOC)litamkubalia mkimbiaji wa mbio za marathon mzaliwa wa Sudan ya kusini sasa kushiriki mashindano chini ya bendera ya shirika hilo na siyo Taifa lake kwenye London 2012.