Mkimbiaji apatikana kutumia dawa za nguvu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mariem Seisouli

Mwanariadha aliyetumainiwa kushinda medali ya dhahabu kwa kasi yake na uhodari katika mbio za mita 1500 Mariem Alaoui Selsouli hatoshiriki mashindano ya Olimpiki kwa kupatikana kua alitumia dawa ya kuongezea nguvu mwilini.

Selsouli mwenye umri wa miaka 28 alishinda medali ya fedha kwenye mashindano ya Dunia mwaka huu alipatikana kutumia dawa iliyopigwa marufuku aina ya furosemid kupitia vipimo vilivyochukuliwa tareh 6 Julai mjini Paris.

Mariam Alaoui amewahi kufungiwa kwa kutumia dawa za kuongezea nguvu mwilini na safari hii huenda akafungiwa maisha.

Katika taarifa yake, Shirikisho la michezo ya Riadha duniani IAAF limetangaza kuwa aina ya dawa ya furosemide iligundulika mwilini mwa mkimbiaji huyo.

"Alaoui Selsouli binafsi aliondoa haki yake ya ukaguzi wa pili na kutokana na hilo amesimamishwa kutoshiriki mashindano yote ya riadha.

Kulingana na Sheria za IAAF bado mwa\nariadha huyo ana haki ya kuomba kesi isikilizwe ambapo chama cha riadha cha Morocco kinatakiwa kuhudhuria.