Soka ya wanawake yafungua Olimpiki

Casey Stoney mmoja wa wanasoka wa Uingereza Haki miliki ya picha BBC World Service

Mashindano ya kwanza yameanza katika Olimpiki ya mwaka huu, licha ya kwamba michezo hii inafunguliwa rasmi hapo Ijumaa. Akina dada wa timu ya soka, Uingereza wanachuana na New Zealand katika mechi ya soka ya wanawake , mji mkuu wa Wales, Cardiff.

Mwandishi wa BBC amesema licha ya iketi chache za mechi hio kununuliwa, mechi ya leo imevutia mashabiki wengi. Mapema leo serikali ya Uingereza ilipongeza hatua ya vyama vya wafanyikazi kufuta mgomo uliopangwa mkesha wa ufunguzi wa Olimpiki na wafanyikazi wa idara ya uhamiaji.

Mgomo huu ulitishia kuvuruga shughuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Heathrow.