Hamilton ashinda mbio za Hungary

Dereva wa Timu ya magari ya McLaren, Lewis Hamilton alijikuta katika sayari yake mwenyewe kwa kuongoza mbio za magari ya Hungary hadi mwisho.

Dereva huyo Muingereza aliweza hata kuweka kasi ya kupindukia kwenye mizunguuko miwili, iliyomuwekea mda wa kuweka pengo la sekunde 0.413.

Dereva wa magari ya Lotus Romain Grosjean alifuata wa pili mbele ya Sebastian Vettel wa timu ya magari ya Red Bull.

Muingereza Jenson Button wa magari ya McLaren alimaliza wa nne, Kimi Raikkonen wa 5, Fernando Alonso akamaliza wa 6 huku Mark Webber akimaliza wa 11.

Nafasi ya 10 ilifunikwa na Felipe Massa wa magari ya Ferrari aliyefuatiwa na Pastor Maldonado wa timu ya magari ya Williams akafuata Bruno Senna, na Nico Hulkenberg wa kikosi cha Force India.

Hamilton alisema baada ya mbio kuwa: "ni afuweni kubwa kuona matunda ya marekebisho tuliyoyafanya na nimefurahishwa kuona kwamba nimelitumia gari ninavyotaka.

Uwezxo wa magari ya Ferrari leo umedhihirisha kuwa magari yao hayana kasi kuyashinda mengine wakati wa ukame, na hilo limepunguza tofauti ya pointi za Dereva Alonzo 34 kutokana na kasi ya magari ya Ferrari yanayofanya vyema wakati wa mvua.