Wilshere atarajiwa Oktoba

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jack Wilshere

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anasema kua mcheza kiungo wa klabu yake Jack Wilshere hatoweza kushiriki mechi za mwanzo wa Ligi kabla ya mwezi Oktoba.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye pia huichezea Timu ya Taifa - England hakushiriki mechi za msimu wa 2011-12 kutokana na tatizo la goti na alifanyiwa upasuaji mnamo mwezi May.

Wenger aliwambia wandishi wa habari kabla ya kukamilisha ziara ya bara Asia mjini Hong Kong kua"Natumai kijana Wilshere atarudi uwanjani October," kabla ya mechi ya mwisho ya Arsenal barani Asia huko Hong Kong.

"wakati Abou Diaby akitarajiwa kurudi, itakua sawa na kusajili wachezaji wawili wapya. Kikosi kitakua imara zaidi na kushindana."

Image caption Wilshere

Wilshere alijeruhi goti lake la kulia na na kufanyiwa upasuaji, lakini akaumia kupasuka kwa mfupa wakati akiuguza goti mnamo mwezi Januari.

Baada ya hapo maumivu ya goti yaliyosibu mda mrefu yaliripuka tena na kumsababishia kijana huyo akose michuano ya Euro 2012.

Wilshere anatarajia kuanza mazowezi mepesi kuanzia mwezi Agosti, kwa kutazamia kurudi uwanjani mwezi Oktoba.

Kwa hiyo ina maana hatoweza kujiunga na kikosi cha England kwa michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Moldova na Ukraine, mapema mwezi Septemba.