Habari za usajili wa Ligi kuu

Habari za usajili Ligi kuu ya England

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Msimu wa usajili

Mwezi Agosti Wigan Athletic

Klabu ya Wigan Athletic imekamilisha usajili kwa kutiliana saini na mchezaji Ivan Ramis kutoka klabu ya Mallorca kwa kitita cha takriban Euro milioni 6. Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 alitarajiwa kujiunga na West Ham baada ya tangazo la Mallorca kudai kua wamekubaliana na West Ham juu ya beki huyo lakini yeye binafsi akafikia makubaliano na Wigan kwa mkataba wa miaka mitatu. Ramis ameichezea Mallorca mara 103 katika La Liga ya Uhispania tangu mwaka 2004. Huyu ni mchezaji wa pili kusajiliwa na kocha Roberto Martinez baada ya Fraser Fyvie kutoka Aberdeen.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Steven Pienaar

Everton Malipo ya Pienaar yaafikiwa

Klabu ya Everton imeafikiana malipo kwa mcheza kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspur Steven Pienaar. Klabu hiyo inayochezea kwenye uwanja wa Goodison Park imekua na hamu kumsajili mchezaji wake hapo zamani ikiwa alihamia Tottenham kutoka Everton mwezi Januari mwaka 2011. Pienaar alirudi Everton kwa mkopo mnamo mwezi Januari mwaka 2012 baada ya kushindwa kufikia viwango vya Spurs. Lakini aliporejea Everton alishiriki mechi 14 akifunga mabao 4 na kuibua kipaji kilichomfanya kuwa nyota katika mwaka 2007.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mmiliki wa QPR

Junior Hoilet ahamia QPR

QPR imemsajili mcheza winga ya kushoto Junior Hoilett kwa mkataba wa miaka minne kutoka klabu ya Blackburn Rovers. Huyu ni mchezaji wa saba kusajiliwa na kocha Mark Hughes, akifuata wachezaji Rob Green, Ryan Nelsen, Fabio Da Silva, Ji-Sung Park, Samba Diakite na Andy Johnson. Kijana huyo kutoka Canada alikua huru bila klabu yoyote baada ya kukataa kutia saini mkataba mpya na Blackburn Rovers, kufuatia klabu hio kushuka daraja hadi mashindano ya Championship.

Vlaar ajiunga na Aston Villa Aston Villa imekamilisha usajili wa beki wa klabu ya Feyenoord Ron Vlaar kwa mkataba wa miaka mitatu akisubiri kukamilisha utaratibu wa afya wiki hii.

Vlaar alikua kwenye kikosi cha Uholanzi wakati wa mashindano ya Euro 2012, na alikua huko Villa Park hivi karibuni kwa majadiliano na kocha mpya Paul Lambert. Beki huyo anatazamiwa kupitia utaratibu wa afya jumatatu kukamilisha usajili wake kutoka klabu ya Feyernoord.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chelsea

Chelsea yakamilisha usajili wa Oscar.

Klabu ya Chelsea imehitimisha usajili wa mcheza kiungo kutoka Brazil Oscar aliyekua akichezea klabu ya Internacional kwa kitita cha Euro milioni €32m. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 yuko kwenye kikosi cha Taifa cha Brazil kinachoshiriki mashindano ya Olimpiki.

Oscar alianza kucheza soka akiwa katika klabu ya Sao Paulo kabla ya kuhamia Internacional mnamo mwaka 2010. Katika kipindi hicho alifunga mabao 11 katika mechi 36 za Ligi.

Chelsea vilevile imemsajili ndugu yake nyota Hazard kutoka Ufaransa aliyesajiliwa na klabu hio mapema Thorgan Hazard.

Haki miliki ya picha
Image caption Luka Modric

Tottenham. Mpango wa Modric kujiunga na Real Madrid bado una ati ati Meneja wa Tottenham Andre Villas-Boas ameonya vilabu vinavyomtaka kiungo wake Luka Modric kua kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 haondoki hadi anayemtaka atimize kitita cha pauni milioni 35 ilichodai Spurs. Kwa kipindi cha mwaka mzima majaliwa ya kiungo huyo yamekua gumzo ambapo Real Madrid imeongoza kwa vilabu vinavyomtaka ajiunge navyo. Lakini Real Madrid imeshikilia msimamo wa kua hawazidishi pauni milioni 27.

Haki miliki ya picha
Image caption Brendan Rodgers

Liverpool yakamilisha usajili wa Borini. Kocha mpya wa Liverpool Brendan Rodgers amekamilisha usajili wake wa kwanza kama meneja wa Liverpool kwa kumsajili mshambuliaji Fabio Borini kutoka klabu ya Roma kwa kitita kama ilivyoarifiwa cha Euro milioni €14. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 huchezea timu ya Taifa ya Italia iliyomaliza michuano ya Euro 2012 katika nafasi ya pili nyuma ya Uhispania iliposhindwa katika fainali.