Ethiopia yazidi kung'ara London Olympics

Tiki Gelana kutoka Ethiopia ameibuka mshindi wa kwanza katika mbio za marathon kilometa 42 wanawake kwa rekodi ya saa 2 dakika 23 sekunde 7 na kupata medali ya dhahabu.

Priscah Jeptoo kutoka Kenya amechukua nafasi ya pili katika mbio hizo akitumia saa 2 dakika 23 nukta 12 na kujinyakulia medali ya fedha. Naye Tatyana Petrova wa Urusi alishika nafasi ya tatu baada ya kutumia saa 2 dakika 23 nukta 29 na kupata medali ya shaba.

Nao Mary Jepkosgei, Edna Kiplagat Ngeringwony kutoka Kenya na Diane Nukuri wa Burundi hawakufanikiwa katika mashindano hayo. Jepkosgei alitumia saa 2 dakika 23 sekunde 56, huku Kiplagat akitumia saa 2 dakika 27 sekunde 52. Naye Diane alitumia saa 2 dakika 30 sekunde 13.