Mwanamke wa Saudi Arabia uwanjani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamasumbwi aliyetoroka

Wanariadha saba kutoka Cameroon waliokimbia kutoka kijiji cha wanariadha usiku wa manane huenda wanatafuta nyumba mpya au fursa bora za kimichezo ,kwamujibu wa afisa wa olimpiki wa Cameroon.

Wanariadha hao waliokuja London wana vibali vinavyowaruhusu kukaa nchini Uingereza kwa kipindi cha miezi sita, na kuongezea kuwa hali kama hii imewahi kutokea kwa vikosi vya Olimpiki na vingine huko Melbourne, Australia na Athens Ugiriki, alisema Taw Taw, afisa mawasiliano wa Cameroon. Akiongezea kuwa mara nyingi hawarudi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Cameroon

Cameroon ilituma kikosi cha wanariadha 37 kushiriki mashindano ya London na wengi wakiwa ni kutoka Timu ya soka ya wanawake wwaliondoka punde baada ya kuondolewa mashindanoni.

Miongoni mwao ni wanamasumbwi watano, muogeleaji na mcheza soka mmoja. Wote walikua wameisha hitimisha mashiondano waliyoshiriki.

Sehemu kubwa ya raia milioni 20 wa Cameroon, huzungumza lugha ya Kifaransa na ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani.

Tataw alisema pia kuwa wana masumbwi watano pia walikua na vibali vinavyowaruhusu kuzuru Ulaya kwa sababu wana viza ya Schengen kutokana na kua walikua wakifanya mazowezi yao nchini Italia kabla ya mashindano.

Hivyo kutokana na urahisi wa kusafiri kihalali katika mataifa ya Ulaya ikiwemo Ufaransa ambako kuna raia wengi wa Cameroon pamoja na familia za wanariadha hao.

Maofisa wa maandalizi ya Olimpiki ya London wamesema kua ingawa Maofisa wa Cameroon wameomba msaada wa kuwatafuta wanariadha wao, bado hawajavunja sheria yoyote bado viza zao zi hai.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sarah Attar

Tukisalia kwenye masuala ya Olimpiki mwanamke wa kwanza raia wa Saudi Arabia kushiriki mashindano ya Kimataifa Sarah Attar amemaliza mbio za mchujo aliposhiriki mbio za mita 800na ingawa alimaliza wa mwisho alishangiliwa na ummati wa watu waliokuepo uwanjani..

Kwa sababu kwa mwanamke kutoka Saudi Arabia, kubwa siyo kushinda wala kuweka rekodi, bali msingi kushiriki..