Ferguson alalamikia Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ferguson

Mkataba wa mchezaji huyo kutoka Uholanzi mwenye umri wa miaka 29, umebaki na mda wa miezi 11 na amekataa kuongezea mda wake akichezea kwenye uwanja wa Emirates.

Sir Alex Ferguson ameiambia BBC kua "tumewasilisha ombi letu kwa Arsenal, lakini wao wamekua wakijaribu kujadiliana na vilabu vingine huku sisi tukisubiri. Sielewi kinachoendelea huko wala sijaweza kupata mawasiliano na viongozi wa Arsenal.

Mara ya kwanza kwa Ferguson kuonyesha nia ya klabu yake kumtaka Van Persie ilikua tareh 20 Julai, na haijafahamika kama wamezidisha kiwango cha fedha walichopendekeza wakati huo.

Inaeleweka kua Arsenal haipo tayari kuanza mazungumzo ya aina yoyote ikiwa upande mmoja unapendekezo la fedha lililo chini ya pauni milioni 20 za Uingereza.

"sielewi mawazo ya Arsenal kwa sababu hawajatoa ishara yoyote," Aliwambia wandishi wa habari baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Barcelona mjini Gothenburg mnamo siku ya Jumatano, iliyomalizka kwa 0-0 kabla ya Barca ishindr kwa 2-0 kupitia mikwaju ya peneti.

Ni vigumu kuelewa jinsi Arsenal inavyoendesha biashara, alizidi kulalamika Ferguson. Sina maelezo zaidi ya kuwafahamisha. Itabidi tuendelea kuwa na subira.

Robin Van Persie kwa wakati huu yuko na kikosi cha Arsenal kwenye ziara ya Ujerumani ambako watacheza mechi ya kirafiki. Meneja wa Arsenal, alisema hivi karibuni kua atajitahidi kuona kua mshambuliaji wake bora anabaki kuichezea Arsenal.

Wakati huo huo, Ferguson alikiri kua alipata kizunguzungu aliposikia kua shabaha yake ya pili Lucas Moura amekubali kujiunga na klabu ya Ufaransa Paris St-Germain. Mchezaji huyo aliyeiwakilisha Brazil kwenye mashindano ya Olimpiki mjini London, atatiunga na PSG mnamo mwezi Januari 2013 kwa mkataba wa miaka minne na nusu kutoka Sao Paulo. Ferguson aliongeza kusema, PSG wamemsajili Thiago Silva na Zlatan Ibramovic, huenda wametumia hadi pauni milioni 150 mwezi uliopita tu.