Mbio mpya za Magari ya Umeme

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 17:21 GMT

Magari ya mbio Formula 1

Katika ulimwengu wa mbio za magari injini inayotegemea joto ndiyo mtawala.

Viwanja vya mduara kwa mashindano ya magari ya Langalanga daima husikika miliyo inayopausa masikio kwa uwezo wa injini zenye nguvu kubwa kama V10 na V12. Ingawa utawala wa injini hizo zinazotegemea joto unakaribia kwisha.

Chama kinachotawala mchezo wa magari FIA, kimetangaza mipango mipya ya mbio za magari iliyobuniwa kwa magari yanayotumiwa nguvu ya umeme pekee.

Mashindano mapya , yatakayojulikana kama Formula E, yanatazamiwa mwaka 2014.

Makampuni yanayotengeneza magari yameombwa kaunde magari yao yenyewe , ambayo yatashiriki mbio za mitaa ya mijini kote Duniani.

Mashindano haya yataendeshwa na shirika la Formula E Holdings, ushirika wa wawekezaji kadhaa wakiongozwa na tajiri mmoja wa Uhispania Enrique Banuelos, aliyetengeneza ma-bilioni ya dola zake kupitia biashara ya ujenzi wa nyumba na kilimo.

Shirika la FIA linasema kua mpango huo ni kuangazia majaliwa ya magari ya baadaye kwa miongo mingi ijayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.