Strauss astaafu mchezo wa Kriketi

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 15:05 GMT

Andy Strauss

Nahodha wa timu ya Taifa ya mchezo wa criketi Andrew Straussamestaafu kutoka mashindano ya aina zote za mchezo huo.

Strauss ameiongoza timu yake ya Taifa kupitia michezo hamsini ya test kati ya mia moja na atakabidhi wadhfa wa nahodha kwa mwenzake Alastair Cook aliyekuwa nahodha wa criketi ya siku moja moja..

Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 35, amesema kuwa kilichosababisha afikie uwamuzi wa kustaafu ni kushuka kwa kiwango chake cha mchezo. Ukweli, aliongezea Strauss, Sijaweza kucheza vizuri kwa mda mrefu sasa. Nahisi kwamba nimeishiwa na mda.

Amekanusha kuwa uwamuzi wake wa kustaafu umeshinikizwa na hatua ya kumtimua Kevin Pietersen kutoka timu ya Taifa.

Strauss ana rekodi ya kushinda mizunguko 7,037 katika mashindano ya Test kwa kiwango cha mikimbio 40.91, hali ambayo inamuweka katika nafasi ya tisa miongoni mwa wachezaji bora wa England wa enzi zote.

Itakumbukwa kuwa ni chini ya uongozi wake kama nahodha ambapo England iliweza kupanda hadhi na kuwa bora duniani kwa mara ya kwanza.

Nafasi yake itachukuliwa na Alastair Cook mwenye umri wa miaka 27 na kibarua chake cha kwanza ni pambano dhidi ya India mwezi Novemba.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.