Man City imemchukua Maicon

Imebadilishwa: 31 Agosti, 2012 - Saa 18:04 GMT
Maicon

Maicon ni kati ya wachezaji kadha wapya watakaoichezea Man City msimu huu

Maicon, aliyeiwezesha Inter Milan kupata vikombe vitatu muhimu mwaka 2010, na ambaye hivi majuzi aliandamwa na majeraha mengi, sasa ataichezea Man City.

Wengi wanaamini siku zake za kung'aa zimepita, lakini kuna baadhi wanaofikiria kwamba Maicon ni kati ya wachezaji bora zaidi wa ulinzi ulimwenguni.

Meneja wa City, Roberto Mancini, aliweza kumfunza Maicon, mwenye umri wa miaka 31, alipokuwa meneja wa Inter kati ya mwaka 2006 hadi 2008.

Mchezaji huyo wa Brazil alianza kuichezea klabu ya Cruziero, kabla ya kuisakatia gozi Monaco, na kisha kuelekea Inter, aliposhiriki katika mechi 235 za ligi ya Serie A.

Maicon atajiunga hivi karibuni na wenzake katika timu ya Man City, mara tu baada ya kipindi kifupi cha mechi zijazo za kimataifa.

Ingawa hucheza nyuma, ana sifa za kushambulia ghafula, na alifanikiwa kuifungia Inter magoli 20, na ameichezea timu ya taifa ya Brazil mechi 70.

Mchezaji huyo mpya wa Man City sasa atakutana na wachezaji wengine waliosajiliwa hivi karibuni katika klabu hiyo ya uwanja wa Etihad, kama vile Scott Sinclair, kutoka klabu ya Swansea, na mlinda lango Richard Wright.

Wachezaji wengine ambao huenda wakasajiliwa na Man City ni kiungo cha kati Javi Garcia na kutoka Benfica ya Ureno, na Matija Nastasic, mlinzi wa klabu ya Italia, Fiorentina.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.