Arsenal yanyoa Liverpool 2-0

Imebadilishwa: 2 Septemba, 2012 - Saa 16:22 GMT

Lukas Podolski

Hatimae Arsenal imeandikisha ushindi wake wa kwanza katika ligi ya Premier msimu huu baada ya kuifunga Liverpool 2-0 nyumbani kwao.

Hii ndio mara ya kwanza kabisa kwa Liverpool kuanza msimu kwa kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wao katika kipindi cha miaka 50.

Magoli yote mawili ya Arsenal yalifungwa na wachezaji wao wapya Santi Cazorla na Lukas Podolski .

Mshambulizi wa Ujerumani Podolski ndiye alikuwa wa kwanza kuipatia Arsenal bao katika dakika ya 31. Na katika dakika ya 68 Cazorla alafanya mambo kuwa 2-0.

Magoli hayo pia ndio yalikuwa ya kwanza kwa Arsenal tangu msimu huu uanze kwani katika mechi zao mbili za awali walitoka sare ya 0-0 na wapinzani wao.

Santi Cazorla

Kufuatia ushindi huo Kocha wa Arsenal alisema kuwa uimara wa vijana wake unaongezeka katika kila mechi na kuwa amefurahishwa na matokeo ya timu yake.

Baada ya kucheza mechi tatu, Liverpool ambayo iko nchini ya mkufunzi mpya Brendan Rodgers ina pointi moja peke yake.

Hii inaweza kufananishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika msimu wa mwaka 1962-63 chini ya Bill Shankly.

Katika mechi hii washambulizi Luis Suarez na Fabio Borini hawakuwa na kubwa uwanjani.

Nae mchezaji mpya wa kiungo Nuri Sahin wa Liverpool pia hakuonyesha makeke yake uwanjani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.