Peacock bingwa wa T44 mita 100

Imebadilishwa: 6 Septemba, 2012 - Saa 22:30 GMT
Jonnie Peacock

Mwanariadha anayekwenda kasi zaidi katika mbio za Paralympics ulimwenguni

Raia wa Uingereza Jonnie Peacock alionyesha uhodari wake katika mbio fupi za T44 mita 100, usiku wa Alhamisi, alipochukua medali ya dhahabu.

Mwanariadha Peacock, ambaye anashikilia rekodi ya ulimwengu, na mwenye umri wa miaka 19, alikamilisha mbio hizo katika muda wa sekunde 10.90.

Oscar Pistorius, kutoka Afrika Kusini, alimaliza katika nafasi ya nne, na matumaini yake ya pekee katika kuondoka na medali ya dhahabu katika mashindano ya Paralympics mwaka huu ni katika mbio za mita 400.

Mmarekani Richard Browne alimaliza katika nafasi ya pili, na Arnu Fourie kutoka Afrika Kusini alishikilia nafasi ya tatu.

Pistorius, mwenye umri wa miaka 25, na aliyepata medali ya fedha katika mbio za mita 200 na dhahabu katika mbio za 4 kwa mita 100, alimsifu Peacock, akielezea ushindi wake "ulikuwa ni kati ya hali ya kusisimua sana katika mashindano ya Paralympics".

"Nilitazamia kuwa miongoni mwa wanariadha watatu wa mwanzo. Lakini tumeshuhudia kati ya mashindano ya kusisimua sana kutoka kwa Jonnie Peacock.

"Mashindano ya mita 100 huwa ni magumu kwangu - mara nyingi mimi hufanya vyema zaidi katika hatua ndefu."

Pistorius atashiriki katika mbio za kufuzu za mita 400 za Ijumaa, na anatazamiwa kuibuka mshindi katika fainali ya mbio hizo siku ya Jumamosi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.