Mkenya David Korir ashinda Paralympiki

Imebadilishwa: 8 Septemba, 2012 - Saa 16:32 GMT

Viwanja vya mashindano ya Olympiki jijini London

Mwanariadha kutoka Kenya, David Korir ameshinda medali ya fedha katika michezo ya walemavu ya Paralypiki jiini London, katika mashindano ya mbio za watu wasioweza kuona, ya T13 ya mita 800.

Wakati wa mashindano hayo Korir alionkeana kuongoza, hadi mwanariadha wa Algeria alipompita.

Hatahivyo alishukuru kwa kupata medali ya fedha.
Amesema mafaniko hayo yamemuinua na inamuwekea msingi wa kusonga mbele.


Aidha amesema atatumia fursa hiyo kuiwakilisha Kenya katika michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil, miaka miine ijayo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.