Van Commenee kujiuzulu

Imebadilishwa: 11 Septemba, 2012 - Saa 13:55 GMT

Kocha mkuu wa riadha van Commenee atajiuzulu kwa timu kushindwa kupata medali za Olimpiki zilizotazamiwa

Kocha mkuu wa shirikisho la riadha nchini Uingereza, Charles van Commenee, atajiuzulu, kufuatia timu yake kushindwa kutia kibindoni idadi ya medali iliyotazamia katika mashindano ya Olimpiki ya London 2012.

Commenee, mwenye umri wa miaka 54, na raia wa Uholanzi, ataondoka mara tu baada ya mkataba wake kumalizika mwezi Desemba.

Van Commenee alikuwa amesema ataondoka ikiwa timu ya Uingereza ingelishindwa kupata zaidi ya medali 8 katika riadha, na angalau moja ya dhahabu.

Licha ya kusifiwa kwa kazi yake, timu hiyo ilipungukiwa kwa medali mbili, na ingawa kati ya medali sita ilizozipata katika Olimpiki, nne zilikuwa ni za dhahabu.

Mara baada ya mashindano, alipoulizwa ikiwa ataendelea na kazi yake, alisema: "Suala la kuaminika ni muhimu sana kwa mtu yeyote yule anayesimamia mpango fulani."

Alichaguliwa kocha mkuu mwaka 2008, hii ikiwa ni mara ya pili kuhusishwa na riadha nchini Marekani, kufuatia timu ya Uingereza kutofanya vyema katika mashindano ya Beijing, Uchina, mwaka 2008, na timu hiyo ilipopata medali moja tu ya dhahabu katika riadha.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.