Hatimae Spurs yafunga

Imebadilishwa: 16 Septemba, 2012 - Saa 18:28 GMT

Tottenham 3-1 Reading

Defoe aifungia Spurs mabao mawili

Mabao mawili ya mshambuliaji Jermain Defoe yalimupa Kocha Andre Villas-Boas furaha kwani ilisaidia Tottenham Hotspurs kuifunga Readings 3-1,siku ya Jumapili.

Huu ndio ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Boas tangu msimu huu uanze.

Ilikuwa ni katika dakika ya 18 ya kipindi cha kwanza ambapo Defoe aliipa Tottenham bao la kwanza kabla ya kufunga lake la pili dakika ya 74 ya kipindi cha pili.

Nae mwamba Gareth Bale akamaliza kibarua alipoipachikia Tottenham bao lake la tatu.

Readings ambao katika mechi hiyo hawakuonyesha mchezo wowote wa haja walijipatia bao la kufutia machozi katika dakika 90 kupita mchezaji Hal Robson-

Ushindi huo wa jumapili ulimpa Villas-Boas afueni kubwa kwani katika siku za hivi karibuni amekuwa na wakati mgumu huku akishutumiwa kwa Tottenham kukosa usndi katika mechi zake zote nne ambazo imecheza.

Kutokana na ushindi huo sasa Tottenham ina pointi 5. Huku Readings ikiwa ya pili kutoka chini baada ya kuzoa pointi moja tu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.