Neil Lennon aisifu Celtic

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 12:48 GMT
Neil Lennon

Meneja Lennon akiinuliwa juu na wachezaji

Meneja Neil Lennon ameisifu klabu yake ya Celtic baada ya Jumanne jioni kuishinda Spartak Moscow ya Urusi 3-2, katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kufuatia ushindi huo dhidi ya Spartak iliyocheza ikiwa na wachezaji 10, Lennon alielezea kwamba anadhani yeye ndiye mtu "aliyefurahi sana barani Ulaya."

"Nadhani siwezi kuwasifu wachezaji hao wa ajabu kwa njia inayoweza kuridhisha," alielezea.

"Walionyesha ubunifu mkubwa na bidii licha ya kulemewa kabla ya mwisho wa kipindi cha kwanza.

"Watu hawatambui kikamilifu sifa za Celtic. Nadhani hatuheshimiwi kadri tunavyostahili, lakini ushindi huo huenda ukabadilisha baadhi ya mawazo kama hayo."

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.