Man City yang'ara tena

Imebadilishwa: 6 Oktoba, 2012 - Saa 15:38 GMT

Manchester City ilithibitisha uwezo wake wa kuendelea kuwa bingwa msimu huu, kwa kuifunga Sunderland magoli 3-0 katika mechi ya Jumamosi.

Aleksandar Kolarov

Kolarov aliiongoza Man City katika kuibwaga Sunderland

Mabao hayo yalifungwa na Aleksandar Kolarov, Sergio Aguero na James Milner.

Bao la Kolarov kufuatia mkwaju wa free-kick uliiwezesha City kuongoza mapema, na mchezaji wa zamu Aguero akaongezea bao la pili katika nusu ya pili ya mchezo. .

Mkwaju wa Milner nao ulimgusa Craig Garnder na kubadilisha mwelekeo hadi kugonga nyavu, na kuiwezesha City kuondoka na pointi tatu.

Wachezaji wa Roberto Mancini walipata nafasi za kuongezea mabao, lakini bila shaka wataridhika na ushindi huo wa magoli 3-0.

Ushindi huo katika mechi hiyo, ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu kwa City kuandikisha ushindi safi kiasi hicho msimu huu, umeiwezesha timu hiyo kuwa katika nafasi ya pili, huku Chelsea ikiendelea kuongoza ligi.

Awali Mancini alikuwa ameelezea wasiwasi wa timu yake kujiweka katika hali nzuri tena ya kupambana katika ligi kuu ya Premier, kufuatia kucheza mechi ya klabu bingwa dhidi ya Borussia Dortmund, Jumatano iliyopita.

Lakini licha ya Mancini kufanya mabadiliko ya wachezaji saba katika kikosi chake, timu hiyo haikuwa na kazi ngumu katika kuhakikisha Sunderland inashindwa kwa mara ya kwanza msimu huu.


BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.