Majeruhi kuiathiri Bafana Bafana

Imebadilishwa: 9 Oktoba, 2012 - Saa 16:38 GMT

Bafana Bafana wana majeruhi kadhaa

Mchezaji kiungo wa timu ya Afrika Kusini,Thulani Serero huenda akakosa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za mwaka 2013 zitakazofanyika nchini Afrika Kusini kutokana na maumivu ya nyonga aliyopata mwezi uliopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye anachezea timu ya Ajax nchini Uholanzi, aliumia wakati wa mechi dhidi ya timu ya ADO Den Haag iliyofanyika tarehe 23 Septemba na hataweza kucheza hadi mwezi Januari mwaka kesho.

" Hatutarajii kupona haraka na kushiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika akiichezea timu yake ya taifa ya Bafana Bafana," umesema uongozi wa Ajax.

"Hata kama atapona haraka, klabu pamoja na mcezaji mwenyewe, inabidi tuwe makini kuhusu hali yake."

Klabu ya Ajax imeongeza kuwa: "Thulani alikumbwa na majeraha madogo madogo msimu uliopita na sasa alikuwa mchezaji wa mara kwa mara kwa timu ya Ajax, kwa hiyo tatizo hili ni gumu kwake."

Kukosekana kwa Serero katika timu ya Bafana Bafana ni pigo kubwa kwa Afrika Kusini, hususan baada ya nahodha wa timu hiyo kutangaza hivi karibuni kwamba anastaafu soka la kimataifa.

Ina maana kwamba litakuwa pengo kubwa kuwakosa wachezaji viungo wawili wa kutegemewa na kutaathiri nafasi ya timu ya Bafana Bafana kushinda katika ardhi yake.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.