Lance Armstrong bado ni mahiri

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2012 - Saa 13:53 GMT
Lance Armstron

Alipokonywa medali saba za ushindi wa Tour de France

Mwendeshaji baiskeli Alex Dowsett wa timu ya Sky, amesema Lance Armstrong ataendelea kukumbukwa kama mwendeshaji baiskeli mahiri ulimwenguni, licha ya madai dhidi ya Mmarekani huyo ya kutumia dawa za kuongezea nguvu michezoni.Shirika la kupambana na utumizi wa dawa za kuongezea nguvu nchini Marekani, lilimpokonya medali zote saba alizokuwa amepata Armstrong katika mashindano ya baiskeli ya Tour de France.

Mwendeshaji Dowsett, kutoka Uingereza, na mwenye umri wa miaka 24, alisema: "Yeye bado ni mahiri katika mchezo huu. Mtu ambaye alikuwa na saratani aliweza kurudi tena katika mchezo, na kupata ushindi wa Tour de France.

"Nadhani yaliyompata sio muhimu, na sidhani ni mambo ya kujali."

Dowsett alijiunga na timu ya Sky mwaka 2011, kutoka timu ya Marekani inayofahamika kama Trek-LiveStrong, na iliyoanzishwa na Armstrong kama timu ya waendeshaji baiskeli chini ya umri wa miaka 23, akiwa na lengo la kukuza vipaji vya waendeshaji chipukizi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.