Sebastian Vettel bingwa Korea Grand Prix

Imebadilishwa: 14 Oktoba, 2012 - Saa 16:59 GMT
Sebastian Vettel wa Red Bull

Sebastian Vettel wa Red Bull

Sebastian Vettel wa Red Bull ameimarisha matumaini yake ya kunyakuwa taji la dereva bora msimu huu wa mbio za magari ya Langa langa baada ya kuibuka na ushindi katika mashindano ya Korea Grand Prix.

Kufuatia ushindi huo, Vettel sasa ametwaa uongozi wa msururu wa mashindano hayo kutoka kwa Fernando Alonso wa Ferrari.

Huu ni ushindi wa tatu kwa Vettel unaomfanya kuwa dereva wa kwanza kushinda mbio nne katika msimu huu.

Dereva mwenzake Mark Webber alimaliza wa pili akifuatiwa na Alonso. Vettel anaongoza kwa pointi sita dhidi ya Muhispania huyo huku kukiwa na mbio nne zaidi kabla ya msimu kukamilika.

Matumaini ya Muingereza Lewis Hamilton kutwaa taji yamekufa baada ya dereva huyo wa McLaren kumaliza nafasi ya kumi.

Kimi Raikkonen wa Lotus alishika nafasi ya tano na kumuondoa Hamilton katika nafasi ya tatu ya dereva bora.

Vettel ana alama 48 mbele ya Raikkonen, na pia sitini na mbili zaidi ya Hamilton, huku kukiwa na alama mia moja tu ambazo bado zipo katika mashindano yaliyobaki ya nchini India, Abu Dhabi, Marekani na Brazil.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.