Marathon ya New York 2012 yafutiliwa mbali

Imebadilishwa: 3 Novemba, 2012 - Saa 10:52 GMT
New York marathon

Mbio za New York hazitafanyika kutokana na uharibifu wa kimbunga Sandy

Mashindano ya mwaka huu ya marathon mjini New York yamefutiliwa mbali, kufuatia uharibifu uliotokea baada ya kimbunga Sandy.

Habari hizo ni kwa mujibu wa meya wa mji huo, Michael Bloomberg.
Kupitia taarifa, alisema: “Hatungelipenda mashindano haya, wala wanariadha watakaoshiriki, kugubikwa na wingu la yaliyotokea, na kwa hiyo tumeamua kuyafutilia mbali.”

Mipango ya kutaka mashindano hayo ya Jumapili kuendelea ilizua malalamiko mengi kutoka kwa wakazi wa maeneo yaliyoathiriwa vibaya mno na kimbunga hicho.

Vifo vya watu 96, na 40 ikiwa ni kutoka New York, inasemekana vilisababishwa na kimbunga Sandy.

Kimbunga hicho tayari kilikuwa kimesababisha vifo vya watu 69 wakati kilipovuma katika eneo la mataifa ya Carribean.

Nchini Marekani, hasa katika pwani ya mashariki, zaidi ya nyumba na biashara milioni 3.5 bado hazina umeme.

Kati ya hizo, milioni 1.2 ni za New Nchini Marekani, hasa katika pwani ya mashariki, zaidi ya nyumba na biashara milioni 3.5 bado hazina umeme.

Kati ya hizo, milioni 1.2 ni za New York, na siku nne baada ya kimbunga, bado hazina umeme.

Ukosefu wa petroli pia kutoka miji ya New York hadi Connecticut ni tatizo kubwa pia.

Katika kituo kimoja cha mafuta, dereva mmoja alikuwa nusra afyatue risasi, kufuatia ugomvi juu ya petroli.

Katika juhudi za kupata suluhu, siku ya Ijumaa, serikali iliamua kulegeza baadhi ya sheria ambazo huzuia matrela ya mafuta kuingia katikia bandari za kaskazini-mashariki.

Mbali na hayo, uongozi wa serikali ya Obama pia umeamua kuagizia galoni milioni 12 zaidi za mafuta (lita milioni 45), na galani milioni 10 za mafuta ya dizeli katika maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Sandy.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.