Craig Levein afutwa kazi

Imebadilishwa: 5 Novemba, 2012 - Saa 19:21 GMT
Craig Levein

Amefutwa kazi kufuatia matokeo duni ya mechi za kufuzu za Kombe la Dunia

Kocha wa timu ya taifa ya Uskochi, Craig Levein amefutwa kazi.

Habari hizo ni kwa mujibu wa chama cha soka cha Uskochi, SFA, mara tu baada ya mkutano na waandishi wa habari.

Levein amefutwa kazi kufuatia matokeo yasiyoridhisha katika mechi za kufuzu kushirikishwa katika fainali za Kombe la Dunia.

Bodi ya chama cha soka cha Uskochi, yenye wanachama saba, ilikutano mwishoni mwa wiki iliyopita, kujadili hatma ya kocha huyo, mwenye umri wa miaka 48.

Levein amefutwa kazi huku ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya kutangaza kikosi ambacho kitacheza katika mechi ya kirafiki wiki ijayo dhidi ya Luxembourg.

Bodi ya SFA ilibidi kukutana, kufuatia malalamiko mengi dhidi ya kocha huyo ambaye aliwahi pia kuwa meneja wa vilabu vya Hearts, Leicester City NA Dundee United.

Levein alikuwa ameapa kwamba kamwe hana nia ya kujiuzulu, na nahodha Darren Fletcher na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Uskochi walikuwa wameelezea hadharani kwamba wangelitaka meneja wao aendelee kuifundisha timu.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.